Ufugaji wa kuku kibiashara ni  mgodi wa dhahabu unaokua kwa kasi duniani na Afrika kwa sasa. Ufugaji wa kuku ni chanzo kikubwa cha ajira katika sehemu nyingi za dunia kwa mfano TANZANIA.

Kuna Zaidi ya ndege million 100 katika mashamba tofauti TANZANIA, lakini hii aiwezi kukidhi mahitaji ya ulaji wa nyama kwa Tanzania ambapo inakadiriwa kuwa na watu takribani milioni 50. ufugaji wa ndege hasa kuku unakua kwa kasi Tanzania na sehemu nyingine za duniani.

Shirika la afya duniani (WHO) limetoa mwongozo kwa watu wote kula nyama nyeupe kwa wingi ukilinganisha na ulaji wa nyama nyekundu,hii ni kwa kufuata kanuni za afya ambapo nyama nyeupe inavirutubisho vingi ukiringanisha na nyama nyekundu na ni nzuri kiafya. Nyama nyeupe ni kama kuku, mabata, bata mzinga. Nyama ya kuku na mayai ni chanzo kikubwa cha protini kwenye mwili wa binadamu.

Pia serekali yetu ya Tanzania imepiga marufuku uingizaji wa kuku na aina ya kuku kutoka nje ya Tanzania, hii ni katika kuleta juhudi za kukuza sekta ya ufugaji kuku kibiashara kuwaongezea kipato.

Kuna vitu muhimu vya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara ya kuku, au ufugaji kuku kibiashara.

Kwanza, watafute wataalamu na ujiunge kwaajili ya mafunzo na upate cheti kama mfugaji ,wenye mafunzo.mafunzo yanaweza kuchukua mwezi mzima kwa njia ya mtandano au uso kwa uso.

Hongera Sana kwa kujiunga KPTL POULTRY SCHOOL kwaajili ya mafunzo ambapo mafunzo haya yatakua ni bure,kwa kuwa tunathamini mchango wako na pia unaweza kuwashirikisha mafunzo haya watu wengine wenye nia ya ufugaji kibiashara wa kuku na kuongeza kipato chao.

Kwa kusema hivyo wanaweza kufanya uchunguzi katika sekta zinazopatiakana katika biashara hii ya kuku ,mfano uzalishaji wa nyama ya kuku,uzalishaji wa mayai,uzalishaji wa vifaranga na chakula cha kuku,uuzaji wa vifaa vya kuku na madawa ya kuku.

Katika hili unahitajika mchanganuo mzuri wa biashara kwaajili ya biashara ya kuku.Mchanganua wa Biashara ya kuku ni ramani bora kwa mfugaji anaenza,ni mwongozo utakao kuonyesha wapi utatoka na utaelekea wapi ili kutimiza malengo yako kwa baadae kwa miaka 2,3,4 kutokana na malengo yako.

Mchanganuo unakusanya , muonekano wa Biashara ya kuku,fursa,mchanganuo wa gharama,faida za mradi wa kuku,uuzaji wa bidhaa za kuku,na malengo ya muda mrefu.

Wataalamu wetu watakusaidia kuata mchanganuo mzuri wa biashara ya kuku baada ya kufanikiwa kufanya stadi ya biashara hii. Tunauzoefu katika uandikaji wa muda mrefu wa miradi ya ufugaji kuku kwa TANZANIA na nje ya nchi. Tupate kwa namba yetu ya whatsapp 0743510033 kupata mchanganuo mzuri wa biashara yako ili upate muongozo mzuri.

Pili unahitaji kupata mahari au eneo zuri kwaajili ya biashara yako ya kuku. Eneo hili ni kwaajili ya kuweka mradi wako wa ufugaji kuku.

Shamba la kuku linatakiwa kuwekwa eneo ambalo si makazi ya binadamu. Harufu inayotoka kwenye shamba la kuku si rafiki kwa mazingira ya binadamu, kwa hiyo shamba la kuku linatakiwa kuwekwa takribani kilomita 10 mbali na makazi ya watu.

Tatu,nyumba ya kukaa kuku inatakiwa kujengwa. Nyumba inaweza kuwa ya ufugaji wa chini ,hii ni nyumba ya kuku inayowapa kuku uhuru wa kutembea kwenye banda , Maranda ya mbao yanatumika kuwekwa chini ya nyumba kama sehemu ya kukanyaga kuku.

Nne ,cage system ni mfumo wa ufugaji kuku ambapo kuku wanawekwa kwenye nyumba ilitengenezwa kwa mfumo wa cage,katika ufugaji huu kuku hawana uhuru wa kuzunguka ndani ya banda. Kuku wanaotaga mayai wanapenda kufugwa kwenye sehemu kama hii.

Baada ya kuweka mazingira ya kuishi kuku salama kitendo kinachofuata ni kutafta sehemu ya kupata vifaranga bora wa siku moja.

Usichukue kifaranga wa siku moja kwa mara ya kwanza bila kumuuliza mtaalamu wa kuku, au fanya usajili katika kiwanda cha kutotoleshea vifaranga.

Kuchukua kifaranga cha siku moja hakikisha umepata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa ufugaji kuku,tunazalisha vifaranga wa siku moja wenye ubora wa kimataifa, unaweza kuwasiliana nasi kwa njia ya whatsapp ili kupata huduma hii kwa idara yetu ya mauzo.

Baada ya hatua hii , weka vifaranga katika makuzi kufikia umri wa kuku mkubwa,kama ni wa nyama hakikisha wanachinjwa kwa wiki 5/6 kulingana na mahitaji ya masoko yako.

Kupata mafunzo kamili au kitabu cha mtandao kuhusu ufugaji kibiashara tutumie ujumbe kwa nambari ya whatsapp 0743 510033 . Tumekuandalia kitabu kwa njia ya mtandao na kwanjia ya kawaida.

Kwa kumalizia , ufugaji kuku kibiashara ni mzuri wenye faida,unaweza kutupata kwa whatsapp namba 0743510033 kwa melekezo Zaidi na mfunzo ya moja kwa moja, ushauri, kupata vifaranga wa siku moja bora kabisa na kuku wanaokaribia kutaga mayai, vifaa vya kufugia kuku vya kisasa,  mchanganuo wa biashara ya kuku au kupata kitabu maalumu cha ufugaji.

Makala hii imeandaliwa na

Dr. JOSEPH L. PAUL

Kukuproject LTD

Josephlucas671@gmail.com