kuku project

Sanjari na faida kubwa inayopatikana katika ufugaji wa kuku kuna mambo ambayo ni lazima ujifunze ili yaweze kukusaidia katika uendeshaji wa biashara ya ufugaji kuku kwa manufaa makubwa. Unapaswa kuhusika kikamilifu katika kujifunza baadhi ya mambo ambayo ni kama muongozo wa miradi ya ufugaji kuku.

Wapo wanaodhani kwamba kuyafikia malengo ya ufugaji mkubwa ni lazima uwe na mtaji mkubwa, hii si kweli. Kikubwa huwa ni malengo binafsi na nia ya kuanza. Ikiwa una  malengo ya kufuga kuku 20000 basi gawa ufugaji wako  kwa mafungu na nyakati tofauti, hii itakusaidia katika kuhakikisha mzunguko wa biashara mfano anza kidogo na kuku 1000 baada ya muda kwa mfano, baada ya miezi mitatu ingiza vifaranga wengine 1000. Endelea kufuga kwa mafungu mafungu mpaka utakapofikia lengo la mradi wako.

Uzoefu utakao upata kwa kuanza kufuga kuku kidogo kidogo

Kujua utunzaji wa kuku kiujumla (management), hii itakusaidia katika kujua shughuli za kila siku za msingi katika ufugaji mfano, ulishaji, ratiba za chanjo, usafi, jinsi ya kuweka rekodi n.k, hii itakusaidia baaadae ukisha anza ufugaji mkubwa ambapo utakuwa una ufahamu juu ya malezi ya kuku kiujumla.

ubora wa mazao ya kuku huchangiwa kwa zaidi ya 90% na utunzaji mzuri

Kuyafahamu masoko, kabla hujafikia ufugaji mkubwa jifunze ni namna gani utaweza kuuza mazao ya kuku wako mfano mayai na nyama. Kupitia kuanza kidogokidogo itakupa mwanga namna gani unaweza kutengeneza faida na namna gani unaweza kulifikia soko ili ukisha fikia uzalishaji mkubwa unakuwa na uelewa na hali halisi ya soko.

kupitia mnyororo wa thamani, utajifunza namna ya kuongeza thamani ya zao katika soko

Kuzijua changamoto na namna ya utatuzi. Ziko changamoto nyingi sana katika miradi ya ufugaji kuku mfano kupitia milipuko ya bei za vyakula unaweza kujifunza kununua chakula kingi kipindi ambacho bei ziko chini. Ziko changamoto nyingi pia katika malezi ya vifaranga ambayo katika kuanza kidogo kidogo unaweza kujifunza na kuwa bora zaidi hapo baadae ukisha anza ufugaji mkubwa.

two happy men carrying chickens
KPTL, tunasaidia wafugaji katika kuzitatua changamoto na kuyafikia malengo yao

Kuhakikisha mzunguko mzuri wa biashara, ufugaji wenye tija ni ule unao zingatia kumtunza mteja au mlaji wa bidhaa yako hivyo kupitia ufugaji wa mafungu mafungu utasaidia muendelezo wa uzalishaji na uuzaji wa mazao ya kuku wako. Mfano utajifunza ni muda gani wa kuleta vifaranga wengine kabla ya waliokuwepo hawajafikia ukomo wa muda wa kutoa mazao.

Shirikisha wataalamu katika kuandaa kalenda ya uzalishaji

Mwisho ningependa kushauri, waone wataalamu wa mradi husika wakupe ushauri kabla hujaanza ufugaji, omba usaidizi wa namna ya uchaguzi wa eneo la mradi, aina ya kuku wa kufuga kulingana na soko lililopo.

“ANZA KIDOGO KIDOGO KWA MIPANGO”

kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba;

0743770771 au 0653691138