1. NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO

Dalili kuu ni Kupinda shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepinda chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani.

KIDERI

Tiba: Ugonjwa huu husababishwa na virusi hiyo sasa HAKUNA TIBA. Kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu.

2. GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.

DALILI KUU:- Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele

TIBA:- Ugonjwa huu husababishwa na virusi vile vile hiyo hauna tiba.

3. MAREK’S DESEASE/ MAHEPE

DALILI KUU:- Kuparalyse /kukakamaa kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia cha chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.

4. NDUI YA KUKU / FOWL POX

DALILI KUU:- Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.

TIBA:- Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic.

5. MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA.

DALILI KUU:- Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za  uso, kichwa  na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.

 6. FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO

DALILI KUU:- Mharo rangi ya njano.

7. COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.

DALILI KUU:- Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.

 8. FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.

DALILI KUU:- kinyesi mharo wa kijani.

9. MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI.

DALILI KUU:- Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.

TIBA:- Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining’iniza juu kidogo.