Leo ningependa ku “share” nanyi walau tujue kwa uchache chimbuko la kuku hawa wafugwao.
Kuku wa kwanza kufugwa alikuwa ni “Redfowl Jungle” miaka 4000 iliyopita. Lengo la kufuga kuku hawa ilikuwa ni kwa ajili ya maonesho ya mapigano na urembo (Cock fighting and beauty competition) kiufupi walifugwa kwa ajili ya michezo.
Kuku waliokuwa wakishinda katika mapambano hayo basi wamiliki wao walipata medali na vitu vingine vya thamani.
Kwa sababu hii kuku wenye maumbo makubwa na kuku wenye rangi nzuri walipendwa zaidi.
Baada ya muda watu wa haki za wanyama wakaingilia kati na kukatisha mashindano hayo, ndipo watu wakaanza kuwauza wale kuku wakubwa kama nyama.
Mwaka 1932 ni mwaka ambao crossbreeding ya kwanza ilifanyika ili kupata kuku wenye sifa mbalimbali, ili kuboresha uzalianaji ndipo wakatokea kuku kwa ajili ya nyama na kuku kwa ajili ya mayai. kimsingi watu waligeukia biashara baada swala zima la kuwatumia kuku kwenye michezo kupingwa.
Mwaka 1950 watu walianza kufuga kuku kwa malengo maalumu na kibiashara. Jambo la kwanza lilikuwa ni kuongeza uwezo wa kutaga mayai kwani Redfowl jungle au kuku wa asili walikuwa wanataga kiasi kidogo sana cha mayai (10 mpaka 12 tu) kwa mwaka. Kupitia zoezi hili kuku wenye sifa mbali mbali walitokea mfano wanao kua haraka, wanao taga mayai mengi, wenye rangi nzuri n.k
Mpaka kufika Mwaka 1990 biashara ya kuku ilikuwa imeshamiri sana kwenye mataifa makubwa kama China na Marekani.Mpaka kufika mwaka. Kwa mwaka 2000 ulimwengu ulikuwa umefikia kufuga jumla ya kuku 14.38 bilion na kufika mwaka 2019 kulikuwa na jumla ya kuku 25.9 billion ulimwenguni kote.
Ulimwenguni kote kuku wanachukua jumla ya 98% ya ndege wote wafugwao, na nyama yake inaliwa kwa 32% ikishika nafasi ya 2 duniani hivyo ikapewa jina la “Universal meat”. kiufupi hiyo ndiyo historia ya kuku wa kwanza kufugwa duniani ambao ndio haswa chimbuko la kuku wafugwao katika ulimwengu wa sasa.
Ahsante kwa kuendelea kufuatilia makala mbalimbali kutoka Kuku Project (T) Ltd.
Wasiliana nasi kwa namba;
0769295782, 0743770771 au 0653691138