Karibu KPTL
Ongeza kipato kupitia mradi wa kuku
Karibu Kuku Project Tanzania Limited (KPTL), kampuni yenye uzoefu mkubwa katika masuala ya ufugaji kuku. Tunajivunia kuweza kusaidia wajasiriamali wengi nchini kukuza na kuendeleza miradi yao ya ufugaji kuku.
Ufugaji wenye tija
Kuku wanalipa!
Ufugaji wa kuku unaweza kuinua uchumi wako na kukufanya uondokane na umasikini. Wafugaji na wajasiriamali wengi wameweza kubadili maisha yao kwa kufuga kuku. Ni biashara rafiki kwa kila mtu na kwa mazingira ya aina yoyote na mahitaji yake katika soko ni makubwa. Kwa kufuata ushauri wa kitaalamu pamoja na kutumia vifaa vya kisasa vya ufugaji kuku, unaweza kuimarisha uchumi wa familia yako na wa taifa kiujumla. Hakika kuku wanalipa!
KUWA KARIBU NASI KUPITIA MAGROUP YETU
Huduma Zetu
Huduma na vifaa vyetu
Ufugaji kuku
Tunafuga na kusambaza vifaranga na kuku bora kama vile Kuroiler na Layers
Uuzaji Vifaa
Tunauza vifaa vya kisasa vya ufugaji kuku kama vile Cages na Incubators
Ushauri
Tunatoa huduma ya consultation kuhusu mbinu bora za ufugaji
Usimamizi
Tupo karibu na wateja wetu kuanzisha na kuendeleza mashamba yao
Our story
Fahamu kuhusu sisi
Kuku Project Tanzania Limited (KPTL) ni kampuni inayojishughulisha na masuala ya ufugaji wa kuku. Kampuni hii ilianzishwa kwa lengo maalum la kusaidia wajasiriamali katika kutatua changamoto zinazowakabili katika ufugaji. Kwa zaidi ya miaka saba, kampuni ya KPTL imekuwa mzalishaji pamoja na msambazaji mkubwa wa virafanga wa kuku aina mbalimbali, pamoja na uuzaji wa vifaa vya kisasa vya ufugaji kuku. Tunao watalaalam katika nyanja mbalimbali za ufugaji ikiwemo washauri, madaktari na wataalamu wa masoko katika tasnia ya ufugaji kuku.